Fizi kuvimba

Ikiwa ufizi wako umevimba, iwe unasikia maumivu au la, ni muhimu kumuona daktari wako wa meno haraka iwezekanavyo ili kupata ushauri wa kitaalamu. Uvimbe wa ufizi ni mojawapo ya dalili za ugonjwa wa fizi (gingivitis), ugonjwa wa fizi ambao unaweza kuendeleza kuwa periodontitis ambapo madhara yake yanaweza yasiwe ya kutibika au kurejeshwa katika hali yake ya awali kiafya. Daktari wako wa meno pekee ndiye ataweza kukadiria ikiwa ufizi wako uliovimba ni ishara ya gingivitis, au ikiwa kuna sababu nyingine inayopelekea hiyo hali. Kwa sababu fizi zilizovimba zinaweza kuletwa na sababu mbalimbali, ambapo kwa ujumla wake ukiwa na hili tatizo unahitaji uangaliwe ili kupunguza hatari ya kulegea kwa meno au kupata maambukizi ya jumla yanayoweza kuwa na madhara kwenye afya ya kinywa na meno.

Sababu za kwa nini fizi uvimba?

Ufizi  kuvimba ni ishara ambayo haipaswi kupuuzwa. Ufizi wenye afya ni wenye rangi ya waridi, na mwonekano wa kama ngozi ya chungwa japo daktari aliesomea anaweza kukusaidia kutambua maana si wakati wote ufizi wenye afya unaweza kuwa na muonekano huo, . Ikiwa fizi zako zinageuka kuwa nyekundu, laini sana, na zimevimba, ni muhimu kwenda kwa daktari wako wa meno kwa uchunguzi. Kuna sababu nyingi za kuvimba kwa fizi.

  • Mabaki ya vyakula kwenye meno na fizi(kutosafisha kinywa vizuri)
    kuvimba kwa ufizi kunatokana na mkusanyiko wa mabaki ya vyakula kwenye meno na chini ya fizi au kingo kati ya ufizi na jino. kutokana na kujazana kwa mabaki na backeria amabo husababisha mishipa midogomidogo ya damu ambayo hupeleka damu na virutubisho kwenye ufizi kupanuka kutokana na maambukizi au kuharibiwa na backeria, ambapo husababisha tishu za fizi kuvimba. Kuvimba huko pia kunaweza kutokana na kuenea kwa bakteria mwilini . Ni muhimu kufanya matibabu ya haraka pale unapoona dalili za gingivitis, ili kuepukana na madhara ambayo yanaweza kuharibu afya ya kinywa na tabasamu au afya yako kimwili. Kufanya hivyo kutasaidia kupunguza gingivitis kukua na kupelekea kupata periodontitis, ambayo inaweza kuwa na madhara makubwa kwenye afya ya kinywa na mwili pia. Ni muhimu kufanya matibabu ya haraka ya gingivitis,itasaidia kuzuia gingivitis kuendele na kuja kuwa periodontitis,  ambayo madhara yake mara nyingi hayawezi badirishwa na hata kukiwa na uwezekano watanzania wengi wameshindwa kumudu gharama hizo
  • Upungufu wa vitamini C
    Upungufu wa vitamini C unaweza kusababisha uvimbe wa ufizi. Upungufu wa vitamini C katika mwili hatimaye husababisha kiseyeye (scurvy). Ni ugonjwa wa mabaharia wa muda mrefu wa siku za nyuma, ambao husababisha kulegea kwa meno kutokana na upungufu wa vitamin C.Unapaswa ufahamu kuwa vitamini C inashiriki katika mchakato wa uzalishaji wa collagen, na virutubisho muhimu kwa kuwa na meno yenye nguvu, ufizi, mifupa ya kinywa kuwa imara.

  • Jipu la kwenye ufizi
    kuvimba kwa ufizi wakati mwingine ni uwepo wa jipu la ufizi.Mrundikano wa usaha kwenye periodontium, yaani eneo lote linalozunguka jino na ambalo linaunda fizi, simenti na mfupa wa alveoli. Mara nyingi hufuatana na maumivu makali. Jipu la periodontal ni hatari hivyo unapaswa uwahi hospitali kwa matibabu ya haraka. Ni muhimu kushauriana na daktari wa meno haraka iwezekanavyo, ili kupunguza maumivu na kuondoa maambukizi kabla ya madhara makubwa unayoweza kuyapata kama picha inavyoonyesha hapa chini.
  • Kuvimba kunakoletwa na matibabu ya meno bandia au upangaji meno

Meno bandia hasa ya kuvaa na kuvua yanaweza pelekea kusugua ufizi na kuleta madhara ya fizi kuvimba ,matibabu ya kupanga meno hasa pale inapokuwa kazi kusafisha vyema meno huweza sababisha fizi kuvimba au hata meno ya moja kwa moja yanaweza kuwa sababu endapo hayakutengenezwa vizuri. Hivyo unapoonana na changamoto yetote wasiliana na daktari alie karibu nawe

Jinsi ya kuondokana na tatizo la ufizi kuvimba?

Ili kupunguza au kuondokana na tatizo la uvimbe wa ufizi wako, jitahidi kumuona daktari wako wa meno, ili aweze kutambua kilichosababisha tatizo na kukupa ushauri wa kitaalamu. Tabia ya kujinywea dawa na kutazamia tatizo ni mbaya na imewaleta matatizo makubwa wengi wa wagonjwa na wengine kuwasababishia kifo au madhara yasiyoweza kurejeshwa. Daktari wako akikuona atakupa matibabu kulingana na sababu na hali ya tatizo lako la ufizi na kwa nini fizi yako imevimba ,picha hapo juu ni moja ya wagonjwa waliopuuzia na kuamua kunywa dawa za kienyeji bila ushauri wa daktari, mgonjwa alipona ila kwa gharama kubwa zaidi kuliko aliyodhani ni gharama mwanzoni ambayo ilikuwa ni ndogo sana

Kama uvimbe wako ni tatizo la awali tunaloita gingivitis basi daktari wako wa meno atakufanyia usafi tunaita scaling then atafanya polishing ili kuondoa (plaque) mabaki ya chakula na tartar. Ikiwa gingivitis tayari imebadilika kuwa periodontitis, matibabu makubwa yatahitajika, utachomwa sindano ya ganzi ili kuondoa uchafu na bacteria walio ndani ya ufizi,baada ya matibabu haya utakubaliana kuwa unakuja kila baada ya muda fulani kuangaliwa na daktari ilikufanya tathmini ya maendeleo ya matibabu yako lakini pia kuhakikisha unafata na kuzingatia usafi ili kuzuia uwezekano wa kurudi kwa tatizo.

Ikiwa una upungufu wa vitamini C, daktari wako atakushauri Kula matunda na mboga mbichi, zenye vitamini C kwa wingi, ambazo zitasaidia kupunguza uvimbe wa ufizi wako au kutumia vidoge vya vitamin C

Jipu la kwenye fizi (abscess periodontal)au alveolitis au maambukizi sehemu uliyong,oa jino , matibabu yatatolewa na utapewa dawa za kuua wadudu(antibiotics) ; katika sababu za kuvimba kutokana na msuguano wa kifaa vya orthodontic (kupanga meno) au prosthesis( meno nübandia), basi dawa za kupunguza maumivu zitasaidia, wakati wa ukisubiri urekebishaji wa meno au vifaa vya kunyooshea meno kinywani mwako.

Related Articles

KUUNGUA

Kuanzia moto wakati wa kukambika hadi chakula cha jioni kilicho pambwa na mishumaa, moto umekuwa sehemu muhimu ya ustaarabu wa binadamu kwa muda mrefu. Hata…

Responses

Your email address will not be published. Required fields are marked *