Afya ya kinywa wakati wa ujauzito 

Ugonjwa wa fizi – gingivitis na periodontitis

Wanawake wajawazito wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa gingivitis, (fizi kutoka damu wakati wa kupiga mswaki) kutokana na homoni za ujauzito zinazoathiri fizi

Ufizi unaathiriwa na plaque(mabaki ya chakula). Gingivitis huathiri hadi 70% ya wanawake wajawazito.

“Uangalifu wa kina unatakiwa katika kupiga mswaki kila jino, [kwa kutumia dawa ya meno yenye floraidi] kwa uangalifu maalum ili kusafisha plaque kwenye  fizi ni muhimu.”

Periodontitis ni aina kali zaidi ya ugonjwa wa fizi unaopelekea kuharibika  kwa tishu na kuyeyuka kwa mfupa ambao hushikilia meno kwa uthabiti. Wavutaji sigara na watu wenye kisukari wana uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa periodontitis. Kwa wajawazito fizi pia huathiriwa na mabadiriko ya homoni wakati wa ujauzito.

periodontitis kali inaweza kuongeza hatari ya:

• kuzaliwa kwa mtoto njiti,mtoto kuzaliwa na uzito mdogo

• pre-eclampsia (toxaemia)-kifafa cha mimba

• Sukari wakati wa Mimba (kisukari wakati wa ujauzito)

“Mimba ni wakati maalum.
Jinsi unavyotunza meno na ufizi wako sasa inaweza kuathiri afya ya mtoto wako na pia afya yako mwenyewe.”

Hadithi za wake wa wazee zimehusisha ujauzito na afya mbaya ya meno – kwa mfano, ‘unapoteza jino kwa kila mtoto unaezaa’. Kalsiamu(calcium) kwa mtoto ‘haikokwi au kuibiwa’ kutoka kwa mifupa na meno ya mama. Walakini, utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kuwa ujauzito husababisha mabadiliko katika kinywa ambayo yanaweza kuhatarisha afya yako ya kinywa.

Homoni za ujauzito

• Mabadiriko ya usafirishaji wa damu kwenye ufizi , na wakati mabaki ya vyakula yapo yanaweza kusababisha gingivitis ya ujauzito – ufizi mwekundu ambao hutoka damu kwa urahisi wakati wa kupiga mswaki na unaweza kuwa laini.

Homa za asubuhi na hamu ya kula inaweza kusababisha:

  • • kuongezeka kwa mashambulizi ya asidi kwenye meno
  • kuongezeka kwa hatari ya kuoza kwa meno

Kufanya Clinic ya afya ya kinywa na meno wakati wa ujauzito

Uchunguzi wa afya ya kinywa na meno mapema wakati wa ujauzito wako itakusaidia kuhakikisha kuwa afya yako ya kinywa iko katika kiwango bora. Ziara ya clinic ya kinywa na meno kabla ya kupanga kuwa mjamzito ni bora zaidi, ili uozo wowote au shida zingine ziweze kutibiwa mapema.

Hakikisha kumwambia daktari wako wa kinywa na meno kuwa wewe ni mjamzito, ili baadhi ya matibabu yaweze kuepukwa.

• Matibabu ya meno kati ya mwezi wa tatu hadi wa sita ndio wakati mzuri zaidi kwako na kwa mtoto wako.

Ni muhimu kudumisha afya ya kinywa wakati wa ujauzito kwa:

• kuzuia maendeleo ya magonjwa ya fizi

• kupunguza bakteria wanaosababisha kuoza kwenye kinywa chako

– utakuwa na uwezekano mdogo wa kupitisha bakteria hizi kwa mtoto wako. Mtoto wako atakuwa na uwezekano mdogo wa kuteseka kuoza meno wakati wa utotoni.

Acha kuvuta sigara

Uvutaji sigara huathiri mwili wako wote pamoja na mdomo wako

– na afya ya mtoto wako itateseka pia.

Kuoza kwa meno

hatari yako inaweza kuongezeka wakati wa ujauzito

• Homa za asubuhi (kawaida katika mwezi wa pili hadi wa nne) mara nyingi husababisha kichefuchefu na kutapika

• Baada ya kutapika:

– suuza kinywa chako mara moja kwa maji au suuza kinywa kwa dawała kusukutua

– kupaka kiasi kidogo cha dawa ya meno kwenye meno yako kwa kidole chako

– usipige meno yako wakati uso wa enamel(layer ya juu) umelainishwa na asidi ya matapishi ya tumbo; subiri kwa dakika 30 hadi uso wa jino urejeshe hali ya awali

• Vitafunio vya mara kwa mara na vinywaji baridi/vinywaji vya kaboni(carbonated drinks) ili kupunguza kichefuchefu, na hamu ya vyakula fulani (mara nyingi vitamu na vinavyonata) vinaweza kuongeza hatari yako ya kuoza meno.

• tema dawa ya meno usisukutue’ baada ya kupiga mswaki

• Kunywa maji ya bomba yenye floridi

– Tunza meno yako na kuzuia kuoza kwa meno kwa kutumia maji ya bomba yenye floridi kwa kunywa na kupikia

• Safisha meno kwa dawa ya meno yenye floridi mara mbili kwa siku

Related Articles

KUUNGUA

Kuanzia moto wakati wa kukambika hadi chakula cha jioni kilicho pambwa na mishumaa, moto umekuwa sehemu muhimu ya ustaarabu wa binadamu kwa muda mrefu. Hata…

Responses

Your email address will not be published. Required fields are marked *