Ugonjwa wa fizi
Angalizo
Kiswahili kinakosa baadhi ya maneno hivyo nitatumia kiswahili na kunasehemu nitachanganya kingereza
Gingivitis na periodontitis yote ni magonjwa ya fizi ila gingivitis ni ugonjwa wa fizi katika hatua za mwanzo ambapo unahusisha fizi pekee na ukiendelea kuathiri fizi na tishu zinazojumuisha meno na fizi unaleta tatizo tunaloita periodontitis ambalo nitatizo linaloathiri fizi na tissue zinazounda fizi na jino
Kulingana na tathmini kwa wagonjwa niliowaona katika clinic nimegundua kuwa watanzania wengi hawafahamu au kujua kuwa wana ugonjwa wa fizi na kama wanafahamu ni kwa kiwago kidogo sana.kati ya wagonjwa watatu niliowahudumia wanatatizo la fizi (gingivitis), hatua ya kwanza ya ugonjwa wa fizi ambao unaweza kwenda periodontal disease. Na jambo la kusikitisha mmoja kati ya kumi huenda kwa daktari wake wa meno wakati ufizi wake unauma na/au unatoa damu. Hata hivyo, gingivitis sio ugonjwa ambao unapaswa kuchukuliwa kwa urahisi. Sio tu inaweza kusababisha periodontitis ikiwa haijatibiwa kwa usahihi na kwa haraka. Lakini muhimu zaidi,ni kuwa inaweza kuwa ishara ya shida kubwa zaidi ya kiafya. Ili kutunza meno yako kwa muda mrefu, na kuwa na afya kwa muda mrefu, ni muhimu kujua jinsi ya kutambua gingivitis au magonjwa ya fizi. Kisha unaweza kushauriana na daktari wako wa meno, ili kufaidika na matibabu mapema.
Ugonjwa wa fizi ni nini?
Gingivitis ni ugonjwa wa fizi kuvimba kwa nje au ndani ya ufizi. Mara nyingi, gingivitis husababishwa na mkusanyiko wa ( plaque) mabaki ya chakula kwenye meno na chini ya ufizi. Bakteria hukua kwenye haya mabaki ya chakula (plaque), na kusababisha kuvimba kwa ufizi. Bakteria ni kawaida katika vinywa vyetu. Bila kutambua, binadamu ana aina 10,000 za bakteria kinywani mwake au zaidi:Japo watafiti wanakadiria kuwa kuna bilioni 50 za backeria katika kinywa cha binadamu. Mara nyingi, bakteria hawana madhara kwa mwili wa binadamu. Kitendo cha namna hii kwa bacteria kutokuwa na madhara katika mwili wa binadamu kinaitwa commensalism, ambapo mwili wetu na bakteria huishi pamoja bila faida yoyote au hasara kwa mmojawapo. Baadhi ya bakteria ni muhimu kwa afya zetu. Kwa hiyo, baadhi ya bakteria waliopo kinywani mwetu hutayarisha usagaji wa chakula hivyo kuwa na faida katika mchakato wa mmeng’enyo wa chakula, na wengine hutulinda dhidi ya vimelea vya magonjwa. Hali nyingine ya mahusiano inaitwa Symbiosis hii ni ya manufaa kwa kila mtu: bakteria hutusaidia kuwa na afya njema, na tunawapa makazi. Walakini, kama ilivyo kawaida,kuna msemo unasema bora ni adui wa uzuri: wakati bakteria huongezeka na kuenea, kinachotokea kuharibu usawa wa asili,ambapo husababisha magonjwa ya uchochezi,yaani ugonjwa unaongezeka palipo na mazalia ya bakteria na moja ya magonjwa ikiwa ni pamoja na gingivitis au ugonjwa wa fizi.
Dalili za magonjwa ya fizi (gingivitis) ni nini?
Ni muhimu kujua jinsi ya kutambua dalili za magonjwa ya fizi ili iweze kumuona daktari na kutibiwa haraka iwezekanavyo.
- Dalili za kawaida za gingivitis ni ufizi unaotoka damu wakati wa kupiga mswaki au kufanya flossing, na ambao fizi huonekana kuwa ni nyekundu sana, kwa kawaida ufizi una rangi ya waridi(pink).
- Kuvimba kwa ufizi, ambayo huchukua mwonekano wa ulaini,kwa kawaida, ufizi wenye afya una mwonekano kama wa granite, kama ngozi ya chungwa.
- Kuwepo wa plaque (mabaki ya chakula) kwenye meno na / au tartar, inayoonekana hata kwa kuangalia kwa macho
- Kuwa na harufu mbaya ya kinywa
Ni mambo gani huongeza hatari ya magonjwa ya fizi (gingivitis)?
Sababu zingine ambazo huongeza hatari ya magonjwa ya fizi (gingivitis):
- kuvuta sigara: Uvutaji sigara husababisha mishipa ya damu kubana, ukiwa na ugonjwa wa fizi mishipa midogomidogo inayoitwa capillaries ya kwenye fizi inakuwa imepanuka kutokana na magonjwa ya fizi hivyo kuvuta sigara husababisha watu wasigundue kuwa wana ugonjwa wa fizi kwasababu ya madhara ya sigara kufanya mishipa hii kusinyaa na inakuja kugundulika kuwa unatatizo la fizi wakati tatizo likiwa limefika mbali.
- Unywaji wa pombe: pombe inasukari ndani yake, na bakteria hula sukari hivyo matokeo yake ni kuathiri fizi
- Msongo wa mawazo (stress): mambo kama kifo, utengano, matatizo ya kitaaluma au ya kibinafsi yanayoleta msongo wa mawazo hupunguza uwezo wa kinga ya mwili kudhibiti bakeria wanao athiri fizi.
- Ulaji mwingi wa vyakula fulani: vyakula vya sukari, lakini pia wale ambao hujitengenezea vitu vinaitwa microlesion kutokana na vyakula vigumu vinavyochubua kwenye uso wa ufizi (haswa chipsi au keki fulani za vitafunio zilizo ngumu).
- Mabadiriko ya homoni: ujauzito au kukoma kwa hedhi husababisha msukosuko wa homoni, ambayo hurekebisha tishu za ufizi. Kubalehe na vipindi fulani vya mzunguko wa hedhi pia vinaweza kuwa na msukumo katika kuchochea maendeleo ya gingivitis. Vidonge vya uzazi wa mpango pia huchochea kutokuwepo kwa uwiano wa homoni na kupelekea uwezekano wa kiwa na tatizo la fizi.
- Kisukari: watu wenye kisukari lazima wazingatie afya ya ufizi wao na afya ya kinywa kwa ujumla. Ugonjwa wa kisukari huongeza hatari ya kusumbuliwa na gingivitis na kisha kukupelekea kwenye periodontitis, ugonjwa wa periodontal unaongezeka zaidi kwa watu wanaoshindwa kucontrol kiwango cha sukari mwilini.
- Matumizi ya baadhi ya dawa: anticoagulants, dawa za kupunguza kinga (zile zinazotumiwa na watu wenye matatizo ya ugonjwa wa autoimmune), watu wanaopatiwa matibabu ya mionzi ni watu wenye hatari ya kupata shida ya magonjwa ya fizi
- Magonjwa : magonjwa ambayo yanayoathiri mfumo wa kinga huongeza hatari ya kuugua magonjwa ya fizi (gingivitis). Hii ni hasa watu wenye maambukizi ya VVU (UKIMWI) hasa wasiotumia dawa za kupunguza makali ya maambukizi, leukemia, mononucleosis, kifua kikuu, maambukizi ya papillomavirus, lymphoma na anemia. Virusi vya herpes pia huongeza kuenea kwa gingivitis, kama vile candidiasis (mycosis kutokana na kuenea kwa Kuvu ya Candida).
- Mapungufu ya vitamin mwilini : ukosefu wa vitamini A, C, B, P, K au D unaweza kusababisha gingivitis ya mara kwa mara.
- Umri: kuzeeka kwa tishu (au senescence) pia huathiri tishu za ufizi, ndiyo sababu watu wazee huteseka mara kwa mara kutokana na gingivitis.
Ni nini husababisha gingivitis?
Kuna sababu nyingi za gingivitis:
Kwa wengi gingivitis ni matokeo ya plaque na tartar -mkusanyiko wa mabaki ya chakula na kugandana kwenye meno na kuingia kwenye fizi. Bakteria aina ya anaerobic (ambao hawahitaji oksijeni kukua) hutumia glukosi kwenye plaque na tartar kuzaliana. Chini ya tartar, bakteria huongezeka na kushambulia tishu za fizi kwa kipindi kifupi au kirefu, na kuzisababishia kuvimba. Mara chache , baadhi ya aina za magonjwa ya fizi gingivitis hazihusiani na uwepo mwingi wa plaque na/au tartar bali huweza sababishwa na ugonjwa wa maumbile, maambukizi ya virusi, magonjwa chochezi ambayo unayo au autoimmune diseases,neoplasms, endocrine, magonjwa ya lishe au kimetaboliki.
Kumuona daktari wako wa meno ili kujua sababu ya gingivitis inaweza kusaidia kutambua patholojia( chanzo au sababu fulani ) wakati ambapo usafi wa mdomo sio sababu ya kuwa na tatizo la fizi. Ni muhimu kutambua dalili za gingivitis na kutibu haraka iwezekanavyo.
kutibu gingivitis au magonjwa ya fizi mapema huizuia kubadilika kuwa periodontitis. Gingivitis inaweza kuponywa bila kuacha athari yoyote. Kwa upande mwingine, periodontitis huacha athari zisizoweza kurekebishwa ikiwepo kupoteza meno yako yote, ambazo zinaweza kubadilisha uzuri wa tabasamu lako.
Kwa hiyo ni muhimu kumuona daktari wako wa meno angalau mara mbili kwa mwaka ili kupewa ushauri na kuangaliwa au kupewa tiba mapema. Lakini juu ya yote, ni muhimu kupiga mswaki meno yako kwa ufanisi na kufuatilia plaque katika kila kona ya kinywa chako kutumia dental floss Kwa njia hii, utaweka meno yako yenye afya na nzuri kwa muda mrefu iwezekanavyo.
Responses